Thursday, February 2, 2012

MAPANGA BADO YAPO SERENGETI


IMARA FOUNDATION hufanya kazi mbalimbali za kijamii kama ilivyo dira yake, tulipata fursa ya kutembelea mojawapo ya Zahanati tulizozijenga mwanzoni mwa mwaka 2000 ili kutoa huduma ya afya kwa jamii kwa kushirikiana na serikali. Tulikutana na kisa kimoja katika kata ya Nyamatoke hapa wilayani Serengeti, ambapo mtu mmoja alijeruhiwa kichwani na panga.


WANAKIJIJI WAMKISHANGAA MAJERUHI KATIKA ZAHATI YA NYAMATOKE






 MKURUGENZI WA IF AKITOA HUDUMA


Mkurugenzi wa IMARA FOUNDATION Dr. Loti Misinzo akitoa huduma kwa majeruhi


HEBU TAZAMA UNYAMAA HUU 
 





 HATATIMAYE NGUVU ZILIMUISHIA KABISA





SAFARI YA KUELEKEA HOSPITALI YA WILAYA ILIANZA BAADA YA HALI YA MGONJWA KUWA MBAYA ZAIDI 






 KUTOKA KATA YA NYAMATOKE MPAKA MUGUMU MJINI NI UMBALI WA KAMA KM 58 HIVI, NA HATIMAYE TULIMFIKISHA KATIKA HOSPITALI TEULE YA WILAYA (NDDH) HAPA MUGUMU MJINI
Mgonjwa alipekwa haraka kuonana na daktari



Daktari wa zamu akipata maelezo sahihi ya mgonjwa


BAADA YA WIKI MBILI TOKEA TAREHE 18 JANUARY 2012 MPAKA LEO TAREHE 2 FEBRUARY 2012 HALI YA MGONJWA NI NZURI








Anaelezea kisa cha kukatwa na panga ni kwamba yeye ni askari wa kijiji (mgambo) mnamo tarehe 18 January 2012 aliagizwa na viongozi wa kijiji cha Nyamatoke kwenda kukamata faini kwa wanakijiji ambao hawashiriki katika maendeleo ya kijiji, baada kufika katika kaya moja alizungukwa na vijana wachache na kuanza kumpiga, na ndipo kijana mmoja aliyekuwa na panga aliaamua kumkata kichwani na yeye kupoteza fahamu. Pia anatoa shukrani za dhati kwa Shirika la IMARA FOUNDATION kwa kuokoa maisha yake kwa kumuwaisha Hospitali.

"SI LAZIMA KUCHUKUA SHERIA MKONONI" ndivyo anavyomalizia kwa kusema.

"SIMAMA PAMOJA KATIKA JAMII"

WATUMISHI WA IF NDANI YA BUTIAMA NA MUSOMA

Muda mwingine tunahitajika kufanya utalii wa ndani ili kufahamu rasilimali za nchi yetu, basi nasi tukaamua kutembelea 'Mwitongo' Butiama alipozaliwa muasisi wa Taifa letu Hayati Mwl. Julius K. Nyerere ili kufahamu historia na mazingiza ya Butiama.



TULIPATA NAFASI YA KUFIMA KATIKA HIMAYA YA CHIFU JAPHET WANZAGI 

Nyumba ya Mwl. Nyerere aliyokuwa akiishi mwanzoni

Mke wa Chifu Japhet Wanzagi akitoa maelezo kuhusu himaya hiyo huku mkurugenzi wa Imara Foundation akisikiliza kwa makini sana











NYUMBANI KWA CHIFU JAPHET WANZAGI 
 
Katibu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT)  Jumanne Magiri na Mke wa Chifu wakiteta jambo fulani



BARAKA ZA WAZEE NI MUHIMU SANA 

" Leo nitawabariki kila mmoja wenu haya karibuni sana wajukuu zangu"





KARIBU MWITONGO WANA IMARA FOUNDATION 


Watumishi wa IF wakiongozwa na mdada ili kupata maelezo kamili ya Mwitongo.


Humu ndipo alipo lala Mwl. Nyerere



 KILA MTUMISHI ANA HAMU YA KUPATA KUMBUKUMBU NZURI 



 MWENGE WA UHURU ULIWASHWA HAPA










TULIPATA NAFASI YA KUWEKA MASHADA KWENYE KABURI LA MWL. NYERERE

Mkurugenzi wa IF Loti Misinzo na Samwel Mewama wakiweka shada la maua katika kaburi


 TULIPATA NAFASI YA KUTOA MAOMBI YETU 








BAADA YA UTALII TULIPATA FURSA YA KUONGEA NA KIJANA WA NYERERE (MADARAKA NYERERE)


Madaraka Nyerere akisiliza presentation yetu toka kwa Mkurugenzi wa IF




BAADA YA MAZUNGUMZO YA DAKIKA 20 HIVI TULIPIGA PICHA YA PAMOJA
 

 TUPO MUSOMA BAADA YA BUTIAMA (TEMBO BEACH)












ILIKUWA SAFARI YA MAFUNZO SANA KWANI ILIONGEZA ELIMU YA MAMBO MENGI KWA WATUMISHI NA KULETA HARI NA NGUVU MPYA YA KUHUDUMIA JAMII.

"SIMAMA PAMOJA KATIKA JAMII"