Thursday, February 2, 2012

MAPANGA BADO YAPO SERENGETI


IMARA FOUNDATION hufanya kazi mbalimbali za kijamii kama ilivyo dira yake, tulipata fursa ya kutembelea mojawapo ya Zahanati tulizozijenga mwanzoni mwa mwaka 2000 ili kutoa huduma ya afya kwa jamii kwa kushirikiana na serikali. Tulikutana na kisa kimoja katika kata ya Nyamatoke hapa wilayani Serengeti, ambapo mtu mmoja alijeruhiwa kichwani na panga.


WANAKIJIJI WAMKISHANGAA MAJERUHI KATIKA ZAHATI YA NYAMATOKE






 MKURUGENZI WA IF AKITOA HUDUMA


Mkurugenzi wa IMARA FOUNDATION Dr. Loti Misinzo akitoa huduma kwa majeruhi


HEBU TAZAMA UNYAMAA HUU 
 





 HATATIMAYE NGUVU ZILIMUISHIA KABISA





SAFARI YA KUELEKEA HOSPITALI YA WILAYA ILIANZA BAADA YA HALI YA MGONJWA KUWA MBAYA ZAIDI 






 KUTOKA KATA YA NYAMATOKE MPAKA MUGUMU MJINI NI UMBALI WA KAMA KM 58 HIVI, NA HATIMAYE TULIMFIKISHA KATIKA HOSPITALI TEULE YA WILAYA (NDDH) HAPA MUGUMU MJINI
Mgonjwa alipekwa haraka kuonana na daktari



Daktari wa zamu akipata maelezo sahihi ya mgonjwa


BAADA YA WIKI MBILI TOKEA TAREHE 18 JANUARY 2012 MPAKA LEO TAREHE 2 FEBRUARY 2012 HALI YA MGONJWA NI NZURI








Anaelezea kisa cha kukatwa na panga ni kwamba yeye ni askari wa kijiji (mgambo) mnamo tarehe 18 January 2012 aliagizwa na viongozi wa kijiji cha Nyamatoke kwenda kukamata faini kwa wanakijiji ambao hawashiriki katika maendeleo ya kijiji, baada kufika katika kaya moja alizungukwa na vijana wachache na kuanza kumpiga, na ndipo kijana mmoja aliyekuwa na panga aliaamua kumkata kichwani na yeye kupoteza fahamu. Pia anatoa shukrani za dhati kwa Shirika la IMARA FOUNDATION kwa kuokoa maisha yake kwa kumuwaisha Hospitali.

"SI LAZIMA KUCHUKUA SHERIA MKONONI" ndivyo anavyomalizia kwa kusema.

"SIMAMA PAMOJA KATIKA JAMII"

1 comment:

  1. THANKS IMARA STAFF FOR LETTING US KNOW ABOUT THOSE PEOPLE WHO SUFFERED FROM LIVED ALIENS

    ReplyDelete