IMARA FOUNDATION hufanya kazi 
mbalimbali za kijamii kama ilivyo dira yake, tulipata fursa ya 
kutembelea mojawapo ya Zahanati tulizozijenga mwanzoni mwa mwaka 2000 
ili kutoa huduma ya afya kwa jamii kwa kushirikiana na serikali. 
Tulikutana na kisa kimoja katika kata ya Nyamatoke hapa wilayani 
Serengeti, ambapo mtu mmoja alijeruhiwa kichwani na panga.
WANAKIJIJI WAMKISHANGAA MAJERUHI KATIKA ZAHATI YA NYAMATOKE 
 MKURUGENZI WA IF AKITOA HUDUMA
| Mkurugenzi wa IMARA FOUNDATION Dr. Loti Misinzo akitoa huduma kwa majeruhi | 
HEBU TAZAMA UNYAMAA HUU 
 HATATIMAYE NGUVU ZILIMUISHIA KABISA
SAFARI YA KUELEKEA HOSPITALI YA WILAYA ILIANZA BAADA YA HALI YA MGONJWA KUWA MBAYA ZAIDI 
 KUTOKA KATA YA NYAMATOKE MPAKA MUGUMU MJINI NI UMBALI WA KAMA KM 58 HIVI, NA HATIMAYE TULIMFIKISHA KATIKA HOSPITALI TEULE YA WILAYA (NDDH) HAPA MUGUMU MJINI
| Mgonjwa alipekwa haraka kuonana na daktari | 
| Daktari wa zamu akipata maelezo sahihi ya mgonjwa | 
BAADA YA WIKI MBILI TOKEA TAREHE 18 JANUARY 2012 MPAKA LEO TAREHE 2 FEBRUARY 2012 HALI YA MGONJWA NI NZURI
Anaelezea kisa cha kukatwa na panga ni kwamba yeye ni askari wa kijiji (mgambo) mnamo tarehe 18 January 2012 aliagizwa na viongozi wa kijiji cha Nyamatoke kwenda kukamata faini kwa wanakijiji ambao hawashiriki katika maendeleo ya kijiji, baada kufika katika kaya moja alizungukwa na vijana wachache na kuanza kumpiga, na ndipo kijana mmoja aliyekuwa na panga aliaamua kumkata kichwani na yeye kupoteza fahamu. Pia anatoa shukrani za dhati kwa Shirika la IMARA FOUNDATION kwa kuokoa maisha yake kwa kumuwaisha Hospitali.
"SI LAZIMA KUCHUKUA SHERIA MKONONI" ndivyo anavyomalizia kwa kusema.
"SIMAMA PAMOJA KATIKA JAMII" 
