Thursday, May 31, 2012

IMARA FOUNDATION NA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Imara Foundation kupitia idara yake ya Elimu na Vijana hufanya shughuli za utoaji elimu kupitia njia mbalimbali kama vile sanaa za maigizo kupitia kikundi cha TEN IN ONE Theater group, michezo ya mpira wa pete, miguu na mikono. Siku ya UKIMWI Duniani IF iliandaa michezo mbalimbali kwa ajili ya kutoa hamasa na elimu kwa jamii ya wilaya ya Serengeti namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa kushiriki michezo mbalimbali.


Uwanja wa mpira wa miguu wa wilaya ya Serengeti   

              



Frank Barnabas (IF staff) na viongozi wa SEFA wakikagua timu kabla ya mechi kuanza kati ya Mugumu FSC na Robanda FSC za wilayani Serengeti.



Frank Barnabas (IF staff) akitoa nasaha, elimu na malengo ya mashindano kwa wachezaji 

Malengo makubwa ya michezo hiyo ya siku ya UKIMWI Duniani ilikuwa ni kufikisha kauli mbiu ya kitaifa  kwa jamii ya wanaserengeti ambayo ilikuwa ni ''Tanzania bila maambukizi mapya, bila unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana'' ila ilikuwa kwa kushiriki katika michezo mbalimbali.

Mugumu FSC

Robanda FSC

Mashabiki wakifuatilia kwa umakini pambano kati ya Mugumu FSC na Robanda FSC 

Washabiki wa Mugumu FSC  


Mugumu FSC washindi wa pambano la siku ya UKIMWI Duniani

Robanda FSC washindi wa pili katika siku UKIMWI Duniani

Mgeni rasmi akitoa hotuba kabla ya kutoa zawadi kwa mshindi wa mechi hiyo.  


Imara Foundation inafanya kazi katika wilaya za Serengeti, Bunda, Musoma vijijini na Tarime. Jiunge nasi katika kusaidia jamii kupitia shughuli mbalimbali.

'SIMAMA PAMOJA KATIKA JAMII'